ONLINE

Friday 19 March 2021

Mbona kaniua

Na Mwende


Maneno yameondoka kinywani mwangu,

Machozi yakakwisha machoni,

Mliposimama kumpigania mtoto wa kike,

Mkanisahau mimi mtoto wa kiume,

Eti linalonikwaza ni,,, sina nafasi tena kwenye jamii.


Kazini mkapa toto la kike kipaumbele,

Wanaoongoza ni wanawake,

 wafanyakazi wengi ni wanawake pia, 

Kosa gani nilililofanya mimi?

Je, mliamua kuniua? 


Sauti sina tena, nguvu 'menipokonya, 

Manufaa ml'otaka mmepata, 

Kama kuniua ni manufaa, 

Nina imani 'meridhika zaidi, 

Taabu iliyopo ni, 

M' tapata mwengine wapi? 


Maumivu  yangu mimi toto la kiume, 

'Meona niyawasilishe kwa maandishi, 

Iwapo masikio yana nta, labda macho yataona, 

Ni haki ninayolilia, nikumbukwe 

Kama si kupewa hadhi, basi nisawazishwe na toto jike

Nifufuke angalau, lakini si kuniua vikali! 

   

                 Mwende 


No comments:

Post a Comment