ONLINE

Thursday 18 March 2021

Maulana wakumbuke

     MAULANA WAKUMBUKE

Na Hosea Namachanja

Rabi uliyetukuka, mbinguni na duniani,

Kote unaheshimika, maajabu pia nyuni

Mapema wakiamka, hukuimbia mitini,

Uhimidiwe hakika, ewe Mungu wa Yusufu


Huwa hawalali njaa, kule kwao kiotani,

Kucha wakikulilia, huwajibu Mkawini

Na mema kufurahia, wanapokula Manani

Uhimidiwe hakika, kwa sababu unatenda


Nalia baba nalia, wasonavyo wakumbuke

Nalia baba nalia, wasafiri, wakumbuke

Nalia baba nalia, waliao wakumbuke

Wakumbuke Maulana, nalia kweli nalia


Nalia kweli nalia, wajane kawakumbuke 

Nalia kweli nalia, wagonjwa kawakumbuke

Nalia kweli nalia, wagonjwa kawakumbuke

Kawakumbuke wagonjwa, nalia baba nalia


Nalia baba nalia, mayatima wakumbuke

Nalia baba nalia, wanafunzi wakumbuke

Nalia baba nalia, na watoto wakumbuke

Nalia baba nalia, kubali maombi yangu


Kuna watu wanalia, nyumba wamefungiwa,

Kuna watu wanalia, wamefutwa kazini

Kuna watu wanalia, wanavurugwa ndoani

Kuna watu wanalia, hawajalipwa mshahara


Kuna watu wanalia, kweli chakula hawana

Kuna watu wanalia, hali zao zinachekwa

Kuna watu wanalia, wanalia tena sana

Ndipo Mola nakuomba, uwasaidie jamani

               

                   Chozi la Kunguni

                    

No comments:

Post a Comment