ONLINE

Tuesday 4 October 2016

Al-Shabaab yatoa video nyingine ya mwanajeshi wa KDF


Kundi la kigaidi la al-Shabaab limetoa video ya pili ya mwanajeshi wa Kenya linalomzuilia tangu lilipotekeleza mauaji ya kinyama El Adde.
Al-Shabaab yatoa video nyingine ya mwanajeshi wa KDF
Mwanajeshi wa KDF aliyetekwa nyara na al-Shabaab.
Mwanajeshi huyo aliyejeruhiwa wakati wa shambulizi la El Adde alielezea masaibu yake mikononi mwa al-Shabaab. David Ngugi Watari alitekwa nyara wakati washambuliaji walivamia kambi ya wanajeshi ya El Adde, Somalia Januari 15, 2016.

Ngugi, mwanajeshi wa kikosi cha 120 cha silaha na zana, KDF, alipoteza jicho moja wakati wa shambulizi hilo lililopelekea wanajeshi wengi zaidi katika historia ya Kenya kupoteza maisha yao.
Ngugi alijiunga na KDF 2009.

Mwanajeshi huyo alitoa wito kwa serikali kumsaidia kuwa huru kwa sababu maisha ya utumwa wa kijeshi hayakuwa mema.

No comments:

Post a Comment