ONLINE

Monday, 29 February 2016

FURAHA GHAYA KWA WANAZUO KUTOKA MAGHARIBI


By WANYONYI Simiyu
1
Shangwe, furaha, vifijo na hekaheka ndizo ngoma zilizomiliki uwanja wa bwawa la Kesses kutokana na ziara ya kimandhari ya wanafunzi wa chuoni humu na ambao hasa ni wakazi wa gatuzi la Bungoma.

Wakiongozwa na Rais wa MUBSA Bw. Werunga Wisdom pamoja na katibu mkuu wa MUSSAS BW. Mwalo Remson Wayne, wanazuo hao walizua filamu ya kufa mtu kwa nyimbo zao za kitamaduni zilizoandamana na densi ya kitamaduni uwanjani humo. Kilicholeta raha zaidi ni kwa wanazuo hao kupata fursa ya kutangamana na mlezi wao Daktari Wanyonyi katika ziara hiyo. Kilele cha furaha hiyo kilifika wakati ambapo waziri wa elimu, vijana na spoti kwenyekaunti Bi Berril Mutekhele alipowasili ili kuwapa nasaha kando na kuchangamana nao kwenye hafla hiyo yakukata na shoka.

Mlezi wao Dr. Wanyonyi aliwashauri wanazuo hao kuwa watumie uwezo wao mkubwa wa elimu hii ya juu kufanya uamuzi mzuri chuoni na kule nyumbani ili kuhakikisha kuwa kaunti ya Bungoma inanufaika hasa kiuongozi kwa jumla. Alimshukuru waziri Mutekhele kwa kuzingatia ahadi ya kuja kutangamana nao ili kuwasikiliza kando na kuyajibu maswali waliokuwa nayo kuhusu mustakabali wa gatuzi la Bungoma kielimu .

Waziri naye kwa upande wake alikuwa na chungu kizima cha ahadi kwa wanazuo hao. Waziri aliahidi kutegua kitendawili cha pesa za bursuries kutoka kwa gatuzi hilo. Kubwa pia ilikuwa ni ahadi ya kutoa mbinu ya usafiri kwa wale wanaonuia kupata kadi za kupiga kura.Aliwashauri vijana hao kujiunga kwenye vikundi anwai vya kibiashara na kilimo ili kupata fursa ya kupata mkopo wa kaunti hiyo. Hata hivyo, alitumia fursa hiyokuwanasihi vijana hao dhidi ya kuwa watu wa itikadi kali na kujiadhari ili wasiingizwe kwenye mtandao wa Alshabab. Aliwahimiza kutumia akili na talanta zao ili kujiajiri bali si kungoja ajira kutoka serikalini. Waziri alisisitiza kuwa serikali ya gavana wa Bungoma Mheshimiwa Ken Lusaka inapigana jino na ukucha ili kuyabadili maisha ya wanakaunti hiyo na kuwaomba waiunge mkono kwa sasa kwani hiyo ndiyo serikali iliyo mamlakani.

Mkono mtupu haurambwi,katika upeo wa mandhari,kulishuhudiwakila aliyehudhuria mandhari hayo ya MUBSAkupata angalau chupa ya maji ili kuzinyoosha koo zao zilizokuwa na mavune kutokana na uimbaji huo na burdani.

No comments:

Post a Comment