ONLINE

Friday 19 March 2021

Mseto wa Habari


Kwaheri Rais Pombe Magufuli


Rais wa Jumuiya ya Tanzania Daktari John Pombe Magufuli ameaga dunia. Akitoa tangazo la kufariki kwa kiongozi huo kupitia stesheni ya TBC, Naibu Rais Samia Suluhu ameelezea kuwa Rais huyo wa awamu ya tano ameaga kutokana na ugonjwa wa moyo, katika hospitali ya Jakaya Kikwete iliyopo nchini humo. Viongozi mbalimbali wakiongozwa na mwenyekiti wa muungano wa muungano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Uhuru Kenyatta, wameendelea kutia rambirambi zao kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania kwa ujumla kwa kumpoteza kiongozi huyo. Magufuli, ameaga akiwa na umri was miaka 61. Amemwacha mjane Janeth Magufuli pamoja na watoto.





Kwaheri Rais Pombe Magufuli


Rais wa Jumuiya ya Tanzania Daktari John Pombe Magufuli ameaga dunia. Akitoa tangazo la kufariki kwa kiongozi huo kupitia stesheni ya TBC, Naibu Rais Samia Suluhu ameelezea kuwa Rais huyo wa awamu ya tano ameaga kutokana na ugonjwa wa moyo, katika hospitali ya Jakaya Kikwete iliyopo nchini humo. Viongozi mbalimbali wakiongozwa na mwenyekiti wa muungano

Uchaguzi mdogo wafanyika Machakos






Wananchi kutoka kaunti ya Machakos, wameelekea debeni kumchagua seneta wao mpya, baada ya kifo cha aliyekuwa seneta was kaunti hiyo Boniface Kabaka mapema mwakani. Ushindani mkali unatarajiwa Kati ya Agnes Kavindu ambaye anagombea kupitia kiti Cha Wiper, na Kengele anayewania kupitia chama cha UDA. 

Magoha atahadharisha watahiniwa wa mitihani ya KCPE na KCSE.

Waziri wa elimu George Magoha, ameelezea taifa kuwa wizara hiyo iko tayari kuwatahini wanafunzi wa mwaka wa 2020 katika darasa la nane na kidato cha nne. Magoha, aliwahikikishia wanafunzi hao kuwa serikali inawatakia kila la kheri, na kuwa mitihani ilitayarishwa kwa kuzingatia hali kuwa wanafunzi kote nchini wamekua nyumbani kwa miezi tisa. Magoha amewaonya watahiniwa dhidi ya kutumia barakoa kuendeleza wizi was mtihani, kwani watapatikana na hatua kali kuchukuliwa dhidi yao. Amewataka wasimamizi was mitihani kuchunguza barakoa za wanafunzi,kabla ya kuanza kwa mitihani yote.

Mwili wa Jeniffer Wambua wapatikana msitu Ngong. 

Mwili wa Jeniffer Wambua, aliyekua Naibu msimamizi katika idara ya ardhi umepatikana katika msitu was Ngong mapema wiki hii, baada ya kupotea kwa Jennifer wiki iliyopita. Upasuaji was mwili uliofanywa na mpasuaji wa serikali  Johannsen Oduor, ulidhihirisha kuwa Jennifer aliaga baada ya kunyongwa. Mwili wake Jennifer ulitambuliwa na familia yake katika makafani ya City. Wachunguzi kutoka kitengo Cha DCI wanatarajiwa kuanzisha uchunguzi baina ya wafanyakazi wenza,kudhibitisha kiini hasa cha kuuawa kwake.

Raila arejea nyumbani kutoka hospitalini

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga, aliruhusiwa wiki hii kurejea nyumbani, baada ya kupata nafuu. Raila, ambaye alipatikana kuwa na virusi vya COVID-19, alikuwa amelazwa katika hospitali ya Nairobi,ambapo alikuwa akipokea matibabu. Katika video iliyosambaa mitandaoni, kiongozi huyo alionekana kuwa afadhali kiafya, huku akielezea nia ya kuendelea kujitenga hadi wakati ambapo atapona kikamilifu.

No comments:

Post a Comment