ONLINE

Sunday 7 February 2021

NIAMINI MAI HANI

    Na Chozi la Kunguni

Miaka nenda na rudi, mambo mengi hutendeka,

Rafiki huwa hasidi, wakatiwe ukifika,

Kama mvua na radi, sautiye husikika,

Penzi kama kikohozi, haliwezi kufichika,


Wapo wengi duniani, ambao umewaona,

Safarini na sokoni, hapo huwezi kukana,

Nami kwangu mtimani,  nakuona wa maana,

Kaniamini tabibu, ndiwe wangu wa pekee,


Ninenapo kishairi, naomba uniamini,

Rohoni nina fahari, kuwa wako mahabani,

Tutazisaka dinari, kila siku maishani,

Ewe ndiwe roho yangu, mke wangu wa thamani,


Chochote unachotaka, mmeo ntakupatia,

Elewa unapendeka, mke wangu nakwambia,

Kwako mie metosheka, mai bebi wavutia,

Siwezi nikachepuka, ili uje kujutia,


Natamani natamani, uje nikukumbatie,

Na uketi ubafuni, busu nikakupatie,

Unilalie kifwani, miguuni nikulee,

 Nikweleze sikioni, nipendavyo usikie,


Mawi sinifikirie, kuwa ninakuchezea,

Hili leo litambue, switi wangu mai dia,

Sinifanye mi nilie, penzi nimekutunzia,

Kama wataka asali, nipo radhi mi kukupa,


Mama wa watoto wangu, nami baba wa wanao,

Sikutakiii machungu, mapenzi  ndiyo kibao,

Nafahamu hulkangu, ukorofi mi sinao,

Hali mimi nakuenzi, sijui nikwambiaje,


Nitakalo mie moja, siku moja nikuoe,

Sitaki viwe vioja, bebi nikakuchezee,

Mambo kweli kuboboja, siyapendi nitambue,

Usiwahi ukadhani, kuwa ninakuchezea,


Ni mbali tumetoana, hili najua wajua,

Mazuri metendeana, hapa chini yake jua,

Wakati tulipatana, ulinamsha hisia,

Kunguni nikadhania, bebi upo chini yangu,


Tamati nikifikia, ninakupenda kikweli,

Si porojo nakwambia, nayosema yakubali,

Kweli ntakuvumilia, aali na kulihali,

Kati ya warembo wote, pekee umenitosha,


 

No comments:

Post a Comment