Mbwembwe na furaha zilitanda
katika kijiji kimoja cha Limpopo, Afrika Kusini, wakati wa sherehe ya
kitamaduni ya ndoa ya mwanariadha Caster Semenya anayegubikwa na utata
kuhusu jinsia yake.
Caster Semenya (kulia) na mchumba wake. |
Caster
Semenya aligonga vichwa vya habari 2009 aliposhinda dhahabu katika mbio
za mita 800 mjini Berlin, Ujerumani. Tangu wakati huo mwanadada huyo
amegubikwa na utata kuhusu jinsia yake halisi.
Semenya
alilazimika kufanyiwa uchunguzi wa matibabu baada ya ripoti kuibuka
kuwa alikuwa na homoni zaidi za kiume kuliko za kike.
Semenya wakati wa harusi yao nyumbani Afrika Kusini. |
Picha za kupendeza za mwanariadha huyo na mpenzi wake wa muda mrefu Violet Roseboya katika harusi ya kufana.
Cha kushangaza ni kuwa wanakijiji
walichangamkia harusi hiyo ya jinsia moja katika bara la Afrika ambalo
ni mwiko kuwa na ndoa za ushoga.
Bingwa huyo wa mita 800 amegubikwa na utata kuhisi jinsia yake. |
Katika sherehe hiyo, Semenya amevalia mavazi ya kitamaduni ya kiume huku mpenzi wake wa kike akiwa na mavazi ya kike.
Ushoga bado ni mwiko katika mataifa chungu nzima ya Afrika. |
Hata
hivyo, licha ya ushahidi wa picha, Semenya amenukuliwa akikana kuandaa
harusi ya kitamaduni ambapo alilipa KSh250,000 kama mahari kwa wakwe
zake.
No comments:
Post a Comment