Na SIMIYU WANYONYI
Ilikuwa ni siku iliyojaa vishasha, mashamshamu, mahanjamu na mishemishe za kila aina chuoni moi kutokana na joto la kisiasa liligubika chuo kizima. Furaha na karaha vilishindana wakati kila jamii ilikutana katika maeneo tofauti tofauti ili kupanga mikakati ya nyumba katika dakika hizi za buriani.
Ilikuwa ni siku iliyojaa vishasha, mashamshamu, mahanjamu na mishemishe za kila aina chuoni moi kutokana na joto la kisiasa liligubika chuo kizima. Furaha na karaha vilishindana wakati kila jamii ilikutana katika maeneo tofauti tofauti ili kupanga mikakati ya nyumba katika dakika hizi za buriani.
COWESA - UPPERHILL(we must great)
Katika uga wa upperhill, jamii ya mulembe ilijumuika pamoja na kutoa msimamo wao kuhusu maswala ya nyumba na uwezekano wa kuunda muungano na yeyote atakayehiari kuwapa watakacho. Katika kongamano hilo, ilibainika wazi kuwa ndoa kati yao na mashemeji haitakuwepo tena baada ya kuhisi kusalitiwa na mashemeji hao. COWESA kupitia kwa viongozi wao, waliamua kwa kauli moja kuwa hawangedhubutu tena kuwashikia ngazi mashemeji kutoka nyanza kwa mara nyingine kwani wao pia wana uwezo wa kujisimamia. Kauli zilizosisitiza msimamo huu ni kuwa, wamekula samaki kwa muda mrefu na umefika wakati wa kubadilisha lishe. Pia waliongeza kusema kuwa maji ya ziwa viktoria yamewazidia. Lililodhihirika pia ni kuwa, upo uwezekano mkubwa wa jamii ya wakalenjin kuungana na wanamulembe baada ya kauli za kunywa maziwa kwa ugali kutolewa sana. Pia, kuwapo kwa Towet Ngetich pamoja na wawakilishi wengine wa jamii ya Kalenjin na hata kuruhusiwa kuongea liliweka wazi azma ya jamii hizi kukumbatiana kwa mara ya kwanza katika historia ya siasa za Moi. Hata hivyo, kuliibuka tetesi kuwa huenda wagombea fulani hasa Husna Hassan wamekwisha tolewa kafara ila tetesi hizo zilipingwa vikali na kudaiwa kuwa ni fununu zisizo na misingi. Hata hivyo, wanamulembe walitoa onyo kali kwa yeyote mwenye nia kumuuza Husna kuwa, huenda wakaamua vinginevyo iwapo tetesi hizo zitakuwa kweli.
Hali haijabainika wazi katika vyeo ambavyo vina wagombea wawili. Cheo cha HEALTH ambapo Faith Chimoli na Juliet Mupalia wameshikilia misimamo yao na vilevile kile cha ENTERTAINMENT ambapo Klint Wafula na John Maina Mwangi pia wanashikilia misimamo dhabiti. Mwanga haujatolewa kuhusu jinsi wagombea hao watakavyochujwa. Kilele cha yote kilikuwa ni nyimbo za kitamaduni wa waluya ambapo pia Towett alijumuika na uimbaji huo kutoka upperhill hadi STUDENT CENTER. Inasemekana kuwa kati ya Towett na Shem, mmoja wao atakuwa mpeperushaji wa bendera ya ndoa hiyo mpya .
Nyuma ya Bweni la A(We the people)
Jamii ya wajaluo ilifanya mkutano wao wa uidhinishaji nyuma ya Bweni la A. Jamii hiyo ilishikilia kuwa ni lazima Rathore Onyango maarufu kama Bishop apeperushe bendera ya CORD. Hata hivyo, baada ya kugundua japo kwa machungu kuwa jamii ya mulembe imeamua kujiunga na wanabonde la ufa, Inasemekana huenda jamii hiyo ikatazamia mlima kenya ili kutimiza matakwa yao.
Tetesi za Ndoa zilizovunjika
Ndoa kati ya Waluo+Waluya na wakisii
Ndoa kati ya Wakalenjin +wakikuyu+wakamba na jamii za Gema
Tetesi za Ndoa zilizozaliwa
Ndoa kati ya Waluya+Wakalenjin +Wakisii
Ndoa kati ya Wajaluo+Wakikuyu+Wakamba na jamii za GEMA
Siku ilitamatika pale ambapo mawe yalianza kurushwa katika ukumbi wa STUDENT center, mahali ambapo Towett na Shem walitarajiwa kutoa hotuba zao.
Je, ni (we the people) au (We must be great)? Ijumaa ijayo ina jibu ya swali hili.
@kaka siwa____amani idumu. Sote tuna damu nyekundu, ngozi nyeusi akili za kufikiria. Zaidi ya yote, sisi ni MAKOMREDI kabla na baada ya uchaguzi. Amani idumu.
No comments:
Post a Comment