ONLINE

Friday 8 July 2016

MUSO SI CORD TENA?

By SIMIYU Wanyonyi

Nguzo kuu za muungano wa CORD zimechukua mielekeo tofauti na isiyotingisika humu chuoni na kutishia nafasi ya muungano huo katika siasa za MUSO mwaka huu.
Umekuwa ni utamaduni chuoni ambapo jamii tatu ambazo ni Luo, Luhya na Kisii huunda ndoa ya pamoja.

Jamii ya magharibi chini ya muungano wa COWESA umeshikilia kuwa ni lazima wapewe kiti kikuu huku zile za nyanza nazo pia, jinsi ilivyojulikana tangu awali, zinamuunga mkono Henry Rathore maarufu kama Bishop. Misimamo hii huenda ikawa kizingiti kwa ndoa nyingine tena.

Fununu zilizozagaa siku ya alhamisi ya kuwa Shem Ouma Wabwire, ambaye ni mgombea wa kiti cha urais kutoka nyumba ya COWESA angelegeleza msimamo wake na kuwania hadhi ya ukatibu mkuu zilipokelewa kwa mitazamo hasi na wanaCOWESA. Wengi wao walisisitiza kuwa, kulingana mkataba uliokuwepo, huu ulikuwa ni wakati wa nyumba ya mulembe kupewa tiketi ya kuongoza baada ya kuwaunga mkono wenzao wa nyanza mara tatu mfululizo ambao ni George Bush (2013),Geoffrey Omondi(2014) na Jared Mogire(2015). Walisema kuwa hawataruhusu kutumiwa tena kama shashi wakati huu na ya kuwa ni lazima wapewe nafasi hiyo.

Ikumbukwe kuwa, katika uchaguzi wa mwaka jana, jamii za nyanza zilichukua zaidi ya robo tatu ya viti vilivyowaniwa huku jamii ya COWESA ikiambulia viwili tu licha ya wingi wao.

Wanamulembe waliongeza kuwa iwapo Shem ataamua vinginevyo, basi ajirushe nje ya kinyang'anyiro kwani kiti hicho cha ukatibu mkuu kitawaniwa na Mwalo Remmy.

Hata hivyo, Shem alipuuzilia mbali fununu hizo akisema kuwa hatatikisika na yuko radhi kupigana jino na ukucha hadi mwisho.

Kwingineko,fununu zinadai kuwa, huenda nyumba ya jamii ya Kisii imetia chini mkataba wa kuungana na JUBILEE na hivyo kujikata kutoka katika muungano huo wa CORD huku jamii ya ukambani ikisemekana kugura na kujiunga na CORD.

Wengi wa wanamulembe wanasema kuwa, iwapo Rathore atashikilia msimamo wake, basi watasimama pekee yao hadi mwisho hata ikiwa itamaanisha kupoteza.

Mgongano huu huenda ukawa ni ufanisi mkubwa kwa Towett Ngetich. Hadi taarifa hizi zilipotayarishwa, jamii za Waluo na Waluya zilikuwa zinaendelea na mikutano yao kinzani katika kumbi za SOWETO MESS na SR 6 kwa usanjari huo.

Je ni we the people au we must be the great?. Jawabu ni julai hii..

No comments:

Post a Comment