Na SIMIYU wanyonyi
Hauchi hauchi unakucha. Hakuna kinachodumu milele eti, kama vingine vyote, binadamu pia hubadililika. Haikutarajiwa. Haikufikirika. Haikuoteka kuwa haya yanayofanyika chuoni , yangetokea. Labda kibwege tu. Mahasimu wawili kuketi chini na kuelewana na kuapa kupanga kazi pamoja. Safari huanza kwa hatua. Hatua ya kwanza labda, ilikuwa ni ile ya Ababu Namwamba na John Waluke. Wakahama katika makazi yao ya muda mrefu.
Siku za hivi karibuni jamii za Kalenjin na Luya, wameonyesha ari ya kuungana na kuunda jabali watakalotumia kulenga na kushinda uchaguzi wa MUSO siku ya ijumaa. Mazungumzo baina ya viongozi wa jamii hizi mbili yameonekana kuzaa matunda kwani, muungano wao sasa umekuwa wazi kama mchana wa jua. Muungano huu ambao hakuna aliyewahi kuutabiria kutokana na historia ya siasa za humu chuoni inasemekana kuwa, umezileta jamii ambazo zinaongoza kwa idadi ya makomredi humu chuoni. Ni muda mrefu tu katika siasa za chuoni ambapo jamii za Luya na Luo pamoja na Kisii, zimekuwa zikiungana dhidi ya zile za Kalenjin, kikuyu na GEMA kwa jumla. Lakini mwaka huu, mkengeuko umetokea. Jamii ya waluya na wakalenjin wameamua kuwa, heri kenda kuliko kumi nenda urudi. Usaliti waliohisi kufanyiwa na wanandoa wa o wa zamani umewaleta pamoja kama yatima waliofiwa. Wameamua kufanya kazi kwa pamoja.
Muungano wao ukaitwa, KALE-LUYHA. Katika muungano huu, kuna vyeo ambavyo vitahitaji majadiliano na vile ambavyo wagombea watachaguliwa moja kwa moja. Katika viti ambavyo wagombea watachaguliwa moja kwa moja ni kama vile:
- Katibu mkuu (sec gen) =Mwalo Remmy (COWESA)
- naibu wa mwenyekiti (VC) =Lavinah Samini(COWESA)
- mwekahazina(finance director) =Murkomen/Newton (KALENJIN)
- msaidizi wa katibu mkuu(ass sec gen) =Festus (KALENJIN)
- michezo (sports & games) = Esther Wasike(COWESA)
- health = Faith Chimoli( COWESA)
Viti vitakavyohitaji majadiliano ya kina ili kuleta maelewano ya ni yupi atakayepeperusha bendea ya KALE-LUYHA ni :
- rais wa MUSO =Shem Albert (COWESA) na Towett Ng'etich (KALENJIN)
- Catering = Husna Hassan (COWESA) na Linet Baliachi(KALENJIN)
- entertainment = Klint Wafula(COWESA) na Dukakis(KALENJIN).
- Security & accommodation =Maxwell Angatia(COWESA) na Kebut Benson (KALENJIN)
Ni matarajio ya wengi kuwa, wale watakaoondolewa kinyang'anyironi wataheshimu uamuzi huo ili kuupa muungano wenyewe uhai na nguvu za kustahimili wapinzani wao. Haijabainika wazi iwapo kuna mpango wa kuileta jamii nyingine katika muungano huu ingawa, wengi wanasema, KALE-LUYHA ina uwezo. Heri nitakula na nini, kuliko nitakula nini. Jamii hizi, angalau zinaona mwanga wa kuaminiana na bila shaka penye nia, pana njia.
@kaka siwa.......heri kujikwaa kidole kuliko kujikwaa ulimi. Chunga ulimi wako usizae tafrani. Amani amani Amani.

Usemi mwelekezi usio na mwenzi. Amani idumu daima
ReplyDeleteUsemi mwelekezi usio na mwenzi. Amani idumu daima
ReplyDelete