ONLINE

Saturday 23 July 2016

HOTUBA YA CHANSELA WA MOI

Julai ishirini na mbili ilikuwa siku muhimu kwa jamii ya Chuo kikuu cha Moi kwa jumla baada ya kutembelewa na chansela wa chuo hiki Muadhamu Profesa Miriam K. Were. Profesa huyo wa afya aliyeanza kazi za kitaaluma akiwa mwalimu wa bayolojia na kemia katika shule ya sekondari mnamo mwaka wa 1965 kabla ya kupitia taaluma kadhaa na kuwa profesa, alichaguliwa kuwa chansela wa Chuo Kikuu cha Moi mwaka wa 2013.

Alianza hotuba yake kwa shukrani kwa mwenyezi mungu na kuonyesha tofauti kubwa kati yake na wasomi wenzake ambao huliona neno la mungu kuwa ni upuzi na kelele. Profesa, aliongoza wanafunzi kwa wimbo wa kumsifu mungu kabla ya hotuba yake kamili.

Hotuba ya profesa ilisheheni mausia kwa wanafunzi na hata uongozi wa Chuo. Aliwapongeza makomredi kwa kupiga kura kwa amani na kupigilia msumari Kauli ya naibu katibu mkuu wa MUSO bwana Festus Koech aliyesema, "demokrasia bila amani si demokrasia". Aliwapa changamoto wanafunzi kuona fahari kujiunga na chuo hiki kwani, kina historia ya kuwa chuo kikuu cha kwanza kuwahi kujengwa eneo la  mashinani. Pia alitaja viongozi wakuu katika siasa ambao ni pamoja na Seneta wa Mombasa Hassan Omar kama vielelezo vikuu vya ukuu wa chuo hiki.

Katika hotuba hiyo, alitaja kuwa elimu siyo uwanja wa kipekee wa kufanikiwa maishani kwani wapo waliofanikiwa nje yake.

Aliishauri hadhira yake dhidi ya ubinafsi na kusema kuwa, ni bora zaidi mtu kutumia uwezo alionao ili kuwainua wenzao walio chini. Alidai kuwa, kipimo bora cha ufanisi wa mtu maishani ni idadi ya watu ambao amewasaidia kuinuka kutoka chini na kuwapa mwelekeo wakati akiwa na uwezo. Aliwasihi wanafunzi kutumia elimu yao ili kuinua wale ambao walikwama vijijini. Alisema kuwa, umuhimu mkuu wa kuwasaidia watu ni kujijengea jina na marafiki wengi.

Kwa upande wa afya, alisisitiza ujumbe wa kuchuja chakula cha kila siku. Alitoa mfano wa matumizi ya nyama kwa sana kama kiini cha kusababisha saratani na kuiomba hadhira yake isiwe na uraibu wa kula vyakula vinavyodhuru afya. Pia, alisema kuwa, inafaa mtu apate muda mwingi wa kulala hasa masaa saba hadi manane ikiwa ni njia moja ya kupumzisha akili na kuongeza uwezo wa kufikiria siku inayofuata. Alizungumzia pia athari ya pombe na dawa za kulevya. Mwisho, profesa aliwarai wanafunzi kutia bidii katika masomo yao.

Kando na hotuba, wanafunzi wengi walimsifu Profesa Were kwa jinsi alivyovaa na kujionyesha mtu aliyeukumbatia uafrika na kujivunia uafrika wake. Hiyo ni changamoto kubwa kwa wasichana wanaoasi uafrika na kujipagaza uzungu licha ya kisomo chao kidigi. Mwendo wa saa sita hivi, profesa alimaliza hotuba yake na kuwaaga wanafunzi.

Follow my blog : simiyukaka.blogspot.com for more Swahili articles and campus news. Twitter  @kaka siwa
Facebook- kaka siwa
       TANGAZO
MERCY CHEPKURUI anakuomba kura ya MUSSAS (VICE CHAIR)
JACOB OTIYA anakuomba kura ya MUESA (Ass sec gen)

No comments:

Post a Comment