ONLINE

Sunday 19 June 2016

Mjue Caster Semenya, Bingwa wa Riadha

.
Mokgadi Caster Semenya kwa jina la kuzaliwa ni mwanariadha wa mbio fupi kutoka Afrika Kusini. Semenya ni mzaliwa wa tarehe saba Januari mwaka wa elfu moja kenda mia tisini na moja mkoa wa Limpopo kule Afrika Kusini. Ana kaka mmoja na dada wawili na imeripotiwa alikuwa na mienendo ya kiuvulana tangu utotoni(tomboy).
Semenya amechukua medali kadhaa za dhahabu na shaba katika mashindano ya riadha ikiwemo kuvunja rekodi ya dunia iliyoshikiliwa na Zelda Pretorius kwa kumaliza kwa muda wa dakika moja, sekunde hamsini na nane na nukta themanini na tano. Caster pia alivunja rekodi ya Zola Budd kwa dakika mbili sekunde sifuri na nukta tisini.
Kufuatua uvunjaji wa rekodi hizi na ushindi  wa medali kadhaa kwa mfululizo ulichangia katika shirika la riadha IAAF kutaka Semenya afanyiwe vipimo vya kujua jinsia yake. Hatua hii ilisutwa na wanahabari, wanasiasa na makundi ya kutetea haki kutoka Afrika Kusini. Hata hivyo matokeo ya vipimo hivyo hayakutangazwa kwa manufaa ya heshima kwa Semenya.
Mwaka jana Semenya alifunga pingu za maisha na mpenziwe wa muda mrefu, Violet Raseboya na wenyeji wa kijiji cha mwanariadha huyo waliisifu ndoa hiyo ya jinsia moja ambayo haichukuliwi vyema huku Afrika. Semenya alivaa mavazi ya kiume huku Violet akivaa vazi la kitamaduni la kike.
Fununu zilitokea mwaka jana kuwa vipimo alivyofanyiwa Semenya, vilionyesha kuwa ana sifa za mwanaume. Imesemekana kuwa Semenya ana korodani( testicles) na hana mfuko wa uzani wala ovari viungo muhimu  kwa viumbe wa kike. Vile vile ana homoni nyingi za kiume ambazo humwezesha kuwapiku wenzake wa kike katika mbio za mita mia nane.
Je, Semenya anafaa kukimbia katika mbio za kike au za kiume?

No comments:

Post a Comment