(Mbele ya jengo la usimamizi wa chuo binti mmoja aliye na ngozi ya majikunde amesimama na bwana mmoja aliyevaa suti ya samawati na viatu vilivyochongeka kwenye sehemu ya mbele)
Sponsa: Utakuwa wapi wikendi hii..
Zainabu: Eeeeh, sijui.. lakini nitakuwa tu chuoni nikisoma.. Kwanza nitakuwa nikifanya mjarabu
Sponsa: Kumaanisha kuwa hutanafasika twende tukauzuru mji wa Eldoret... Kisha utarejea chuoni
Zainabu: Akhi sitaweza hata..na sioni haja kuzuru Eld.. Tena sina hela..kwa hivyo siwezi
Sponsa: Mmmh! Naona akili zako zimekwama kwake Sadiki
Zainabu: Eti Sadiki..ni wewe uonaye hivyo!
Sponsa: Yule ni ndoto mbaya ambayo haifai kusimuliwa wala kutajwa hapa. Wamwonaje?
Zainabu: Akijifanya kuwa hakumsikia.. Nani?
Sponsa: Akikasirika Kumbe uko nami kimwili tu na mawazo yako umeyawekeza kwake. Yaani Sadiki.
Zainabu: Sioni chochote cha kuzungumziwa kumhusu Sadiki!
Sponsa: Ala! Kuuuumbe! Hata baada ya kukutunza vizuri na kukufanya ukawa mwanamke kamili umenigeukia. Kumbuka hata hela za chumba nakulipia...
Zainabu anatabasamu na kuangalia chini
Na hayo ni madogo. Nitakulipia karo na kukununulia simu mpya aina ya Infinix 345A Nataka uingie katika kikundi cha mabinti ambao wako "first class"..
Zainabu: Pole dia, tuliachana na Sadiki kitambo sana. Hata nambari yake ya simu nilipangusa. Mbona unamfikiria Sadiki badala ya kunifikiria mimi....nifikirie mimi. Unampenda Sadiki ama mimi.
Sponsa: Sponsa anacheka na kuyaanika meno yake machonge yaliyotoka nje ya mdomo wake.
Wajua Sadiki hawezi kutekeleza haya yote. Hata kukunulia hata vibanzi vya shilingi kumi. Mbona ukamfuate jamaa kama huyo. Mavazi mazuri pia hana,sio wamwona kila siku akiwa amevaa ile sweta yake nyeusi iliyo na mavaka meupe.
Zainabu: Nilikuambia unifikirie mimi.. Anasita kidogo Siku yangu ya kuzaliwa ni Ijumaa wiki kesho.. Na hujanipa habari zozote kuhusiana na taarifa hiyo..
Sponsa: Nikuambia uniachie hayo. Usiwe na wasiwasi. Lakini kumbuka pia mimi hujanijibu..
Zainabu: Kuhusu jambo lipi?
Sponsa: Kuhusu kuenda kuzuru Eldy.. Nataka tuondoe ukinaifu wa humu chuoni. Tuionje baridi ya mji wa Eld.. Kisha Jumatatu tuje kuhudhuria mhadhara...Anamtazama na anagundua kuwa hajachangumka ... Changamka nawe..Ondoa baridi
Simu ya Zainabu inakiriza, anaitoa mfukoni na kutazama ili aone mpigaji. Anaijibu na kuweka simu sikioni.
Sadiki: Hello Zainabu.. Siku nyingi hatujazungumza?
Zainabu: Mie ni mzima..niambie umenipigia
Sadiki: Sina maneno ila ningependa kesho utenge muda ili tukakutane. Haifai kwa wapenzi kuchukua muda kabla ya kuonana. Waonaje Zainabu?
Zainabu: Akhi sidhani endapo nitanafasika... Naenda kumsalimia shangazi yangu mjini Eld.. Yule shangazi yangu niliyekuambia anaishi Eld..
Sadiki: Ooh lakini sio ungeahirisha..pengine tungeenda tukatembee falls
Zainabu: Kule vichakani tunaenda kufanya nini? Kule hata nyoka aweza kukung'ata..Wasichana wengine wanapelekwa majijini wewe wanipeleka misituni.
Sadiki: Nawe,ninatamani ni uwezo ndiwo sina. Ntakamilisha kisomo hivi karibuni kisha ntajenga nyumba nzuri na kununua gari nzuri. Ili tuishi nawe kwa furaha. Unambiavyo hivyo waumiza moyo wangu.
Zainabu anakata simu na kusonya.
No comments:
Post a Comment