Timbe na Johanna wadidimiza ndoto za Congo.
Baada ya kutoka sare ya bao moja dhidi ya Tanzania na Sudan mtawalia, vijana wa nyumbani walijikakamua na kung'aa hapo jana. Itakumbukwa kuwa ndiyo mechi ya kwanza ya kocha Stanley Okumbi kupata ushindi baada ya kupoteza dhidi ya Guinea Bissau. Kenya ni ya mwisho katika Kundi E huku ushindi wao dhidi ya Congo ukiwapa Guinea Bissau tikiti ya kufuzu kwa fainali za AfCoN.
Congo walipata uongozi dakika ya kumi na tisa kupitia kwa mkwaju wa penalti uliofungwa na Prince Oniangue baada ya Ismael Gonzalez anayechezea uhispania kufanya dhambi katika kijisanduku cha penalti. Dakika tano baadaye, Ayub Timbe alifanya Nazi take vyema na kusawazishia vijana wa nyumbani.
Kabla ya bao hill, Wanyama alikuwa amemwandalia Michael Olunga pasi murua lakini walinzi wa Congo walikuwa macho kabisa kuondoa hatari ile. Baadaye Olunga alijaribu kufunga tena ingawa kombora lake halikulenga shabaha. Dakika kumi kabla ya mapumziko, Timbe anayechezea Lierse karibu afunge la pili lakini kipa wa Congo alifanya uokozi mwafaka.
Kenya walitoka kwenye chumba cha mavazi na nguvu mpya huku nahodha, Victor Wanyama akifanya mashambulizi kadhaa kabla ya Erick Johanna kufunga bao la ushindi dakika ya sitini na saba. Kocha wa timu ya taifa Stanley Okumbi amehimiza wakenya kushabikia timu hiyo kwa vile kuna dalili ya mafanikio hivi karibuni huku nyota kadhaa kama Eric Ouma almaarufu Marcelo wakiibukia.
Ligi ya hapa Chuoni Moi yang'oa nanga.
Ligi ya hapa chuoni ilianza siku ya Jumamosi huku mfadhili mkuu Mwanaspoti Mike akitwaa kombe kwa mshindi wa ligi hiyo.Timu kadhaa zitang'ang'ania taji hilo ambazo ni; Field Marshals, Wayia FC, Ted FC, Sharks, Soweto, Blues, Classical Sportiff, Alahli na Angaza FC. Mechi kadhaa zilisakatwa wikendi hiyo huku talanta anuwai zikidhihirika.
Jumamosi
Soweto vs Angaza 1-1
Blues vs Classical 1-1
Field Marshals vs Wayia 4-0
Sharks vs Ted 6-0
Jumapili
Blues vs Angaza 0- 1
Classical vs Ted 5-0
Wayia fc vs Soweto 0-1
Mechi hizo zitaendelea wiki hii kutoka siku ya Alhamisi.
No comments:
Post a Comment