ONLINE
Tuesday, 31 May 2016
GUMZO LA MAKOMREDI
( Micro-komredi anatambaa juu ya kitanda. (Komredi-jinale machana anafungua mlango na kuingia huku mkononi amebeba vitabu)
Micro-komredi: Hahaha.... leo umehudhuria mhadhara...
Komredi: Umewahi nisikia nikisema kuwa sitahudhuria mhadhara.. Chuoni nilikuja kusoma bwana si kufanya masihara...
Micro-komredi: Eti wewe ulikuja kusoma? Nilikusikia siku ile ukimwambia rafiki yako sijui eeeeh...Omondi kuwa ulikuja chuoni kujivinjari..
Komredi: Chuoni tunajivinjari na kusoma...hayo yote ni mamoja...hujajua sheria ya makomredi?
Micro-komredi: aaah si ni ile nasikia mnasema eti "a comred is always right.." nilisikia mkisema siku moja. Ninapojificha godoroni huyasikia mazungumzo yenu..mbona hamjawahi kufanya maandamano eti tunawasumbua?
Komredi: Alaa! Wewe ndo' uliniharibia usingizi leo...
Micro-komredi: Ulidhani ukiwasha stima ningejificha...ni kweli nilijificha lakini sikuenda mbali. nilikuwa hapo tu karibu. Nilikusikia ukisema eti afadhali ungebook hostel H..
Komredi: Huko ni afadhali....
Micro-komredi: Huku mnalia, kule H makomredi wenzako wanaomboleza..
Komredi: Mtakomeshwa siku moja..mtanyunyuziwa dawa iliyo na sumu
Micro-komredi: zi, Wapi,hizo ni ahadi tu mlipewa kuwa tutanyunyuziwa sumu. Nilidhani umefahamu hali ya mambo chuoni Moi. Hiyo dawa itanunuliwa mwaka kesho na watasema imegharimu mamilioni. Wakati huo utakuwa umeondoka chuoni. Utakuwa huko nje ukila githeri ukisubiri ajira.Hehehe...Chuo kilicho na utofauti ati! Chuo chenye upekee!
Komredi: Wewe,usianze uchokozi!
Micro-komredi: Usinikasirikie yakhe! sisi sote ni makomredi hata kama mimi micro-komredi.... Sote huweza kusema "Riiah"
Komredi: Unajua kusema Riiah hata wewe?
Micro-komredi: Mie husikia tu mambo. Nilisikia mkisema hivyo wakati wa uchaguzi...mbona hao waliokuwa wakiwaambia "Riiah" hawajachukua hatua...Wako wapi hata salamu pekee hawawasalimu....mlijiita eti..We the people..."
Komredi: Nani alikuambia wametusahau,ngoja mgomo utokee utajua kuwa tuliwachagua kwa sababu...hatukuwachagua kwa kuchagua tu.
Micro-komredi: Elimu ya chuo kikuu haijakusaidia? "You have gone through the university but the university have not gone through you" nadhani umepevuka kimawazo? Hao viongozi wenu huwatumia ili wakapewe donge nono..wajinga ndo waliwao...
Komredi: Unaita makomredi wajinga..
Micro-komredi: Namaanisha kuwa upevu wa kimasomo wanao ila kwa masuala ya kawaida, hamna tofauti kati yao na walevi kijijini...
Komredi: Usitusi komredi bwana...ujinga wa makomredi u wapi bwana?
Micro-komredi: U kwenye uchaguzi hasa..wakati wa uchaguzi utawaona nje ya ukumbi wa students centre. Utawasikia wakiulizana makabila ya wale wanaogombea....Eti waunde miungano ya kisiasa,miungano ya kikabila.
Komredi: Tukome masihara sasa... mpenzi wangu akija hapa usimtaabishe sio?
Micro-komredi: Nitashirikiana nawe ukiniahidi jambo moja.
Komredi: Jambo lipi hilo! Nipo radhi. La mno uamue kujificha demu wangu akija hapa
Micro- komredi: Naomba unifunze kusema "riiah"
Komredi: utaweza kweli? Jitayarishe basi tuseme kwa pamoja..moja,mbili,tatu...
Micro-komredi na Komredi: Comraaaaaaaaaaades Riah!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment