ONLINE

Monday, 11 April 2016

UMBILE LAKO AULA



Ni dhahiri, uzuri wako ni dhahabu
Ni shahiri, kwangu wewe ni dhawabu
Si shari, wakitaka wengi penzi kuwatibu
Ni shwari, ukiwaeleza ninakumiliki.

Natazamia, siku ile utauchukua
Mkono wangu, unambie 'mekuchagua'
Na moyoni, kitendawili kakitegua
Hadi mwisho, kama wanandoa tutakua

Nashangaa, mbona mungu kakuumba
Kaamua, kakuleta kwetu Bungoma
Na halafu, kwa kunipenda ukaamba
Nimetambua, kwa ajili yangu uliumbwa

Nafurahia, nikikuona ukitembea
Na wako mwili, kiuchuzesha nakuselea
Nakukazia, macho yangu yakulowea
Nafahamu, unajua wanipendeza.

Mguu wako, kama mche umeviringika
Mikono yako, kama pamba melainika
Kiuno chako, kama tausi chapendeza
Amini Felly, nikikwambia nakhuyanza

Kifua nacho, kama miba kimesimama
Macho nayo, kama ua yanavutia
Midomo nayo, kama perememde yatamanisha
Amini Felly, urembo wako haulinganishwi

Ukiniona, tafadhali tabasamu
Ukiniota, tafadhali unisalimu
Ukinishika, tafadhali unibusu
Ninaamini, Felly wangu ananiyanza
            Ndakhuyanza sana!

No comments:

Post a Comment