Nalia, nalia kilio cha chozi la mliwa. Sijui iwapo nitawahi pata msamaha kutoka kwa mamangu mzazi na ndugu zangu. Japo alinienzi kwa dhati ya moyo wake,kutokana na tukio hilo lililonisibu ilimbidi apoteze imani yake kwangu.
Nilipojiunga na chuo kikuu, watu wa mlango wangu walikuwa na matumaini mengi kwangu hasa baada ya kukamilisha kisomo changu na kuwa mwalimu wa sekondari na baadaye kuendeleza masomo yangu na kuwa mhadhiri ningewafaa. Hiyo ndiyo iliyokuwa ndoto yangu, ndoto ambayo nilitamani itimie. Angalau aushi yangu ibadilike. Nione jua na mwanga mkuu hatimaye. Walijua na kusadiki bayana kuwa, ningebadilisha kurasa zao za maisha na hali.
Lakini haikuwa hivyo asilani, nilisahau kile ambacho kilinipeleka chuoni walahi. Hii hali haikuja tu hivi hivi, ni baada ya kucheza na cheche za moto. Nao moto ukawa radhi kutekeleza wajibu wake. Ni kama mtoto aliliaye wembe kisha hatimaye imkate. Je, atamlilia nani? Hivyo ndiyo ilivyokuwa.
Nilipokutana na Rukia, tulichumbiana naye kwa hiari na mapatano. Tukaahidiana kuchanjiana chale kama ithibati ya usuhuba wetu. Tukalitekeleza pasi kuboronga wakaa. Kitu kilichonichochea kuzama katika bahari yake ya mapenzi nikiwa uchi ni kuwa kwetu na kwao si kitalifa kirefu. Yeye yuaishi mtaa wa Mwembe tayari na mimi Shimo la Tewa. Niliona heri kumchumbia kwa dhati ya moyo wangu.
Baada ya muda mfupi alinitaliki. Nilibaki kwa dhiki kuu. Nilimthamini kama pumzi ya moyo wangu na tukawa tumeahidiana kuwa tutaoana halafu.
Madai yake ya kunitupa jongoo na mti wake yalikuwa eti nilikuwa simfaidi kwa hela za matumizi ya kila uchao. Kwake ikambidi amsake mwenzi mwengine. Kama kawaida tulikuwa tumefanya naye tendo. Akawa amenisalihishia ukimwi kama hedaya. Likizo zote sijarejea nyumbani. Naona haya, fedheha imenitinga. Wacha nifie huku kuliko kuwastaabisha watu wa nasaba yangu. Ama nifanyaje?.........................
No comments:
Post a Comment