ONLINE

Monday 7 March 2016

⚽⚾πŸŽΎπŸŽ±πŸ‰πŸˆπŸ€ JUKWAA LA MICHEZO



Na WANYONYI Simiyu

Afc leopards yaichachafya Gor mahia

Licha ya kuwa na kikosi kichanga zaidi kwenye historia yao, mabingwa mara kumi na tatu wa ligi kuu ya KPL A. F. C leopards ilisakama bingwa wa ligi ya sportpesaGor Mahia bao moja kwa bila. Bao hilo lilifungwa na Lamine Diallo kunako dakika ya themanini. Ushindi huo umechupisha Ingwe hadi nafasi ya kwanza huku Gor mahia wakisalia katika nafasi ya kumi na mbili bila ushindi wowote.

Leicester city yatanua mwanya kwenye EPL

Bao la kimuujiza la Riyad Mahrez dakika ya hamsini na sita lilipanua mwanya kati ya kiongozi wa Epl Leicester na nambari mbili Tottenham hadi alama tano. Tottenham kwa upande wao walitoka sare ya mabao mawili na wachezaji kumi wa Arsenali. Arsenal walisalia wachezaji kumi baada ya Francis Coquelinkuonyeshwa kadi nyekundu.Chelsea ilitoka sare ya bao moja na Stoke.

Ronaldo atamba kwenye La liga
Nyota wa Real Madrid Christiano Ronaldo alifunga mabao manne na kuisaidia Madrid kuishinda Celta Vigo mabao saba kwa moja.Mabao mengine yalifungwa na Jesse Rodriguez, Gareth Bale na Pepe. Kwingineko viongozi wa ligi hiyo Barcelona waliishinda Eibar mabao manne bila jibu. Lionel Messi alifunga mabao mawili huku Suarezna Munir El Haddadi wakifunga bao moja kila mmoja.

MKUSANYIKO WA MATOKEO YA WIKENDI

SPL

Gormahia 0-1 Afc Leopards

Bandari 1-0 Sony sugar

Ushuru 0-1 Ulinzi stars

Rangers 1-0 Sofapaka

Chemelil 0-0 Nairobi city stars

Muhoroni 1-2 Tusker

Western stima 1-1 Thika united

Mathare 0-0 kakamega homeboyz

EPL

Crystal Palace 1-2 Liverpool

Watford 0-1 Leicester

Chelsea 1-1 Stoke city

Everton 2-3 Westham

Man City 4-0 Aston villa

Newcastle United 1-3 Bournemouth

Southampton 1-1 Sunderland

Swansea city 1-0 Norwich

Tottenham 2-2 Arsenal
West bromwich 1-0 Man United

No comments:

Post a Comment