ONLINE

Wednesday 2 March 2016

JUKWAA LA MICHEZO



By YASSINA Terry

Adhabu kwa K'Ogalo ; Kenya yashindwa kung'aa

Mabingwa wa ligi kuu ya Premier nchini,Gor Mahia wamepigwa faini ya shilingi laki moja baada ya kukosa kutuma ratiba yao kule Madagascar kwa wakati. K'Ogalo walipigwa faini hiyo wakati wakichuana na CNaPS kule Madagascar kwa mkondo wa pili wa mechi za kuwania ubingwa was Afrika(CAF).Gor walipoteza mechi hiyo na kubanduliwa kwenye michuano hiyo.
Ripoti kutoka kwa usimamizi wa kandanda nchini( FKF) zimekiri kuwa kamati hiyo imo tayari kulipia Gor Mahia faini hiyo kwa vile CAF haitambui klabu. Kwa kweli Kenya ilifeli kwenye mechi hizo baada ya timu zote mbili zilizoshiriki kubanduliwa michuanoni na timu ambazo wangebandua.
Licha ya kukamilisha msimu bila kupoteza mechi yoyote, K'Ogalo ilicharazwa na CNaPS mabao mawili kwa moja hapa nyumbani kabla ya kupoteza tena bao moja kwa nunge kule Madagascar. Bandari nayo ilipoteza mawili kwa nunge dhidi St Lupopo kutoka Demokrasia ya Kongo kabla ya kutoka sare ya bao moja kwa moja hapa nyumbani. Hata hivyo, kiini cha matokeo hayo hakijabainika.

Mabao kumi na saba yapatikana;Mathare United yang'aa

Jumla ya mabao kumi na saba yalifungwa wakati wa mechi za ligi kuu nchini wikendi iliyopita. Baadhi ya mabao hayo yalipatikana wakati wa mechi ya Sofapaka dhidi ya Mathare United Jumamosi iliyopita.Mabingwa wa ligi hiyo Gor Mahia, Bandari, Ulinzi Stars na AFC Leopards hawakushiriki kwenye mechi hizo kwa vile walikuwa wanaliwakilisha taifa katika mechi za kitaifa.
Mathare United ilitua juu ya jedwali baada ya kuwanyuka Sofapaka mabao matano kwa mawili. Timu hiyo ambayo mkufunzi wake ni Francis Kimanzi ilishinda kufuatia mabao ya Obadiah Ndege, Erick Johanna, Noah Abich na Roy Syamba.
Batoto ba Mungu chini ya ukufunzi wa David Ouma, walipata mabao mawili ya kufutia machozi kupitia kwa Brian Nyakan na Heritier Luvualu. Sofapaka imo nafasi ya kumi na moja kwenye jedwali.
Timu ya Tusker ilinyakua ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Nairobi Stars .Mabao ya Tusker yalipatikana kutoka kwa Humphrey Mieno na Ekaliani Ndolo huku Eugene Asike akijifunga. Muhoroni Youth ilinyuka Thika United mabao mawili kwa moja.

No comments:

Post a Comment