Screenshot of won ID sms. Photo: JEMEDARI |
MORE BY THIS WRITER
Kucheza kamari umekuwa mrimo wa kila siku kwa wenyeji wa nchi hii ili angalau kupata riziki ya kila siku. Mchezo huu nchini Kenya umekuwa kama ajira kwa walioajiriwa na waso' na kazi. Kwa mvuto huu wa soko kubwa na la haraka, kampuni nyingi za kucheza kamari zimejitokeza ili kunufaika na gulio hili. Kampuni za sportpesa, Elitebet, M-cheza, Betway ni baadhi ya kampuni zilizoshusha mizizi yao kwenye mifuko ya mcheza kamari.
Sportpesa ndiyo kampuni maarafu kwenye gulio hili. Kampuni hii imekuwa maarufu kiasi cha kupata pesa za kuthamini Ligi kuu nchini na vile vile kuthamini miamba wa soka nchini AFC LEOPARDS na mabingwa wa ligi Gor mahia.
Uking'wafua mnofu, ukumbuke kugwengwenya mifupa eti. Wacheza kamari huwa na hili akilini ndiposa utapata kwenye usemezano wao misimu kama; risking na sure bet. Hili linadhibitisha ukweli wa kuwa mshindi yeyote huwa na bahati bali si ubabe wa mtu katika kujua historia na uchambuzi wa michezo.
Ajabu ni kwamba kuna wenzetu ambao wamecheza mchezo huu bila kufanikiwa. Wanateka maji kwenye jabali. Wengine hufikia kiwango cha kutaka kusitisha uwekezaji wa kila siku kwenye kampuni hii ya sportpesa lakini jinsi mhimili wao mkuu huwa, gamblers never quit, imani yao huzidishwa mara kwa mara waonapo wenzao wakishinda. Imani yao huwa ni bahati kama ajali, huitambui siku ya kuja. Labda siku moja itawanyea ya baraka.
Wengine husema 'sport pesa inanyonya', ni ukweli? Sina shaka kuwa kampuni hii imesaidia sana wanafunzi hasa wa vyuoni kupata angalau kikombe cha chai ili kuishtaki njaa na hata kulipa karo ya chuo. Vile vile, imesababisha kupunguka kwa tofauti kubwa iliyokuwepo awali kati ya tajiri na maskini kwani waweza mdharau maskini kwa saa hii, lakini baada ya dakika tisini huenda akawa millionaire. Hili linawafanya walalahoi wasidharau kiserema kwani pia ni jembe. Aina ya simu inayotuma arafa si hoja,hoja ni bahati uliyonayo. Hata "mulika mwizi" yawezakupa milioni.
Manufaa makubwa hasa ni kupunguka kwa visa vya kujitia kitanzi miongoni mwa mashabiki wa soka ya Uingereza hasa wale wa Arsenal na Man United. Nangoja kuona ikiwa mashabiki wa mashemeji watajitenga dhidi the ya kuzua vurugu na kurusha mawe viwanjani iwapo harara itawazidia. HEWALA!
No comments:
Post a Comment