ONLINE

Thursday, 25 February 2016

GHARAMA YA WANAHABARI



By SIMIYU Wanyonyi

Hii leo kwenye soko la Moi tuzamie gharama ya mwahabari. Huyu ni mtu aliyeitikia wito kutoka kwa mwenyezi;witowa kumwomba aje duniani na kuchukua vitushi vya matukio ya wanadamu na aviweke wazi mbele umati ili wanaofaa kurekebishwa warekebike kwa aibu. Kama mwenyezi mungu apendavyo kanisa ambalo ni sisi binadamu tunaomwabudu, alituma kioo duniani ili yeyote anayetaka kujitathmini kiutanashati au kiufaafu ajitazamie kwenye kioo bila kuudhi wenziwe kwa maswali. Kioo hiki nacho alikisafisha kiasi kwamba kikirukiwa na tope, dunia nzima itafahamu hilo na kukisikitikia. Mwanadamu yeyote anayempenda mwenyezi mungu, sharti akiheshimu na kukitunza kioo hiki kwani ndicho msema kweli. Ndicho humweleza anavyoonekana kwa sasa, humpekulia mambo asiyoyaona kwa urahisi, humvumbulia mapya asiyojua na hatimaye kumtabiria atakavyofanana ikiwa atauruhusu uzee umwathiri. Hiki ni kioo, msema kweli duniani;mpekuzi wa yaliofichika.
......... kwa konzi na fimbo eti huko ni kumtuzua

Walimaliza wahenga waliponena, ukistahi mke ndugu huzai naye.Mwanahabari kama kioo cha jamii, hukiuka mipaka ya unyamaume na kujitosa katika utumwa wa mkamambogo bila kujali ubabe wake. Wakati mwingine hata huumeza moto ilhali macho yake ya' wazi, akili zake zi' timamu na sifa zake za urazini zikimsukuma. Huingia kwenye kichuguu cha mchwa na suti yake ya kuzaliwa ,kwenye chaka la duma na kwenye pango la simba, hamadi iliyo kwenye kibindo chake ikiwa ni kalamu na karatasi tu;Kunakili, kuandika na kujisahihisha makosa ahisipo kuwa hajachukua usemi mzuri wa taarifa. Yote hayo hufanya yeye kwa kusudio la kupinga methali ya koko haidari maji. La mno ni kumwonyesha mwananchi, msomaji, mtazamaji na msikilizaji, mambo yatendekayo kwenye pango la nyoka au kiotanimwa njiwa. Kuwapasha habari. Huo ndio mrimowe kutoka kwa mwenyezi mungu.
Ajabu ni kuwa, kwa gharama hiyo yote, kando na kuwa ni mwitikio wa wito, kuna wana wa wafalme na hata wafalme kwenye himaya zao ambao humwona mwanahabari kuwa ni vazi chakavu linalopaswa kutupwa au kuchomwa. Wengine wanamwona kama ngoma ya kuchezwa kwa konzi na fimbo eti huko ni kumtuzua. Kama wasihiri, wengine humwona yule yule mwanahabari kuwa ni izraili aliyetumwa kumharibia starehe. Badala ya kumchukua kama kalamu ya kujisahihisha, wanamwona kama wino wa kukuza maandishi ya uovu wao.
Mjumbe hauawi eti.Usijipagaze uchachandu kujipalia makaa kwa kukivunja hiki kioo cha Rabana. Ili kulihanikiza jina lako koteduniani, utamhitaji yule mwanahabari. Ili kutangaza biashara yako hata ikiwa haramu, mwanahabari atakufaa. Ili kusafisha jina lako baada ya kupakwa urojo wa msala, ni yule yulemwanabari atakuja na kukumwaia marashi ili uvundo utokomee. Kama wasemavyo;mtunze punda akutunze, mheshimu mwanahabari akusahihishe kwani gharama yake huitambui wala kuing'amua. Alaaniwe yeyote anayepaka tope na anayekivunja au kukikwaruza kioo cha jamii.
Taamali
Waja uma kumi usipate hata kimoja

No comments:

Post a Comment