ONLINE

Monday 27 June 2016

KAULI MBIU YA COWESA!



COWESA ni muungano wa wanafunzi wote wanaotoka magharibi ya Kenya walio hapa chuoni Moi.Inajumuisha kaunti za; Vihiga,Busia,Kakamega,Trans nzoia na Bungoma.
         Wanafunzi hawa waliandaa mandari siku ya Jumamosi saa tano asubuhi, agenda kuu ikiwa ni kujadili hatima ya wagombea wao katika mchakato mzima wa siasa za MUSO.Wanagenzi hao waliitikia mwito wa mwenyekiti wao Sharon Muhonja na kufika kwa wingi katika eneo maarufu la "Moi falls" ili kuonyesha umoja wao katika nyumba ya Mulembe.
        Wagombea waliokuwepo walijumuisha Shem Ouma mgombea katika wadhfa wa mwenyekiti,Lavina Samini mgombea katika naibu mwenyekiti,Remmy Wayne- Katibu mkuu,Jay Mwangi na Clinton Wafula,Chimoli Faith na Juliet Mupalia wakiwania nyadhfa za masuala ya burudani na afya mtawalia.
      Siku ilianza kwa densi za chini kwa chini na miondoko ya kila aina.Nyimbo za kitamaduni zinazoimbwa katika sherehe za jando pia hazikusazwa.Mwacha mila ni mtumwa,hili lilidhihirika wazi kutokana na ukwasi wa wanafunzi hao wa miondoko ya kitamaduni.Ngoma ikichezwa sana bila shaka hupasuka, kasheshe za densi zilifikia kikomo saa sita mchana.
      Katika mkutano wao walizungumzia maswala mengi yakiwamo jinsi ya kunyakua wadhfa wa mwenyekiti katika halmashauri ya MUSO.Waliapa kutobadili msimamo wao na kuahidi wadhfa huo hawatapeana kwa marafiki zao wa muda ambao kwa sasa pia wameonekana kuwa na msimamo mkali.Wengi wa wanachama walizungumzia amani na ushirikiano kama njia bora ya kuafikia malengo yao.Wanazuo hao walionyesha kuridhika kwao kwa hatua iliochukuliwa na Mwenyekiti wa COWESA na kuahidi kushirikiana kwa hali na mali msimu huu wa uchaguzi,kwa kusaili vita vya panzi furaha kwa kunguru.
      Sharon Muhonja ambaye ni mwenyekiti alisema kuwa umefika wakati ambao ni lazima historia ibadilishwe kwa kuchukuwa wadhifa wa Mwenyekiti katika uongozi  wa MUSO.Aliwasihi wagombea wengine wajitahidi ili waweze kupata tiketi ya kuwania nyadhifa mbalimbali wakati wa kuunda muungano."Tutawapa tiketi ya muungano wagombea walio na umaarufu na uungwaji mkono pekee,"Sharon aliapa . Aliwaonya wanachama waasi na kuahidi kufanya juhudi za kibinafsi ili kukabiliana nao bila kuogopa wala kutishwa.alimalizia kwa kuomba amani na ushirikiano ili kuafikia malengo yao waama umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.
       Kilicho na mwanzo hakikosi mwisho,shughuli nzima iliishia katika ukumbi wa wanafunzi kwa shangwe na bashasha zilizowavutia wengi.Waliteremsha vinywaji ili kupanguza ukavu katika koo zao na hatimaye kutawanyika huku kauli mbiu ikiwa "WE MUST BE GREAT " iliyoasisiwa na Shem Ouma anayegombea wadhifa wa Mwenyekiti.

No comments:

Post a Comment