ONLINE

Saturday 2 April 2016

GARISSA MEMORIAL: Wakenya Waadhimisha Kumbukumbu za Shambulio

Kusanyiko la watu katika bewa kuu la chuo kikuu cha Moi 
Maelfu ya Wakenya kutoka maeneo tofauti nchini siku ya Jumamosi walikongamana katika chuo kikuu cha Moi bewa la Garissa na bewa kuu Eldoret  ili kuadhimisha mwaka mmoja tangu shambulio baya la kigaidi lililowauawa wanafunzi 147.

Usalama uliimarishwa ndani na hata nje ya chuo hicho huku wale waliokuwa wakiingia wakifanyiwa ukaguzi mkali na maafisa wa polisi.

Vilevile mamia ya watu walishiriki katika mbio za marathon za kumbukumbu ya shambulio hilo.

Waliohuduria ukumbusho katika chuo cha Garissa wakiongozwa katika mbio za nyika na mbunge wa eneo hilo Bw. Duale (kofi nyeusi)

Viongozi wa eneo hilo wakiongozwa na mbunge wa eneo hilo pamoja na kiongozi wa walio wengi bungeni Adan Duale walishiriki katika mbio hizo za kilomita 5.

Waandalizi wanasema kuwa mbio hizo zililenga kuleta uwiano kati ya Wakenya kufuatia shambulio hilo.


Maadhimisho hayo yamehusisha uzinduzi wa mnara wa ukumbusho.

No comments:

Post a Comment