ONLINE

Wednesday 9 March 2016

MERIMELA HAJAFA BADO?


BY SIMIYU WANYONYI

Asemwaye sana haelewi ati. Ni kweli? Katika maisha yetu ya kila leo tunajishughulisha na maswala mengi;yenye kuleta faida, ya hasara na ya kujiburudisha maadamu tupo duniani. Siku nyingi ikiwa umefwatilia na kusoma toleo langu mwenzako, matini yangu husheheni mtindo wa maisha humu chuoni. Labda kuna sababu, sijatambua hilo bado.

Mtoto wa kike alidhaniwa kuwa kiumbe dhaifu. Mwanamke aliumbwa kama msaidizi tu kulingana na dini yangu. Huku kulimfanya awe chombo cha kumpembeja mwanaume na kukamilisha sala zote anazohitaji mwanamume. Akiwa kwao nyumbani kabla ya ndoa, alitunzwa na kufunzwa njia za kuishi na mumewe. Mapishi yake yalichujwa na mamaye ili aendapo kwa mtemiye ahakikishiwe maisha. Siku hizo, ijapokuwa yasemekana kuwa mwanamke alikandamizwa kihaki, kwa upande mwingine alitibiwa sawa sawa kinidhamu. Hizo ni zama za chanjagaa al'ejenga nyumba kakaa.

Kwenye karne hii ya ishirini na moja, uhuru wa mke umetangazwa paruwanja. Sheria zimebuniwa kuhakikisha kuwa dhana ya bibilia inapingwa kwa dhati. Kivipi lakini? Eti mwanamke asawazishwe na mwanamume. Hilo ni wazo zuri kwa kuwa binadamu ni ngeu na mifupa ila usawa huu una mipaka. Nangoja kusikia siku moja kuwa 'mke amepachika mumewe mimba na baada ya miezi tisa mume alazwe kwenye chumba cha Leba. Hapo nitasadiki kuwa mwanamume na mwanamke ni sawa.

Uhuru wa mwanamke nao umezua makuu ya kushitukiza. Uhuru huu wameuhanikiza hadi kwenye hazina kuu ya ndoa. Tunda hilo ambalo 'nasikia'ni tamu kuliko halua limekuwa kama chemsha kinywa asubuhi na chajio giza lipishwapo. Ni kweli tunda hili ni tamu ndiyo maana lafichwa na kutolewa tu wakati na mahali maalum, lakini je unalitoa kwa mtu maalum. Wanadada wengi wangekuwa riwaya ya kiswahili, riwaya hiyo ingesheheni wahusika wengi wakuu. Labda watatofautiana tu kiwakati na mandhari lakini wanafanya tendo kuu. Wanazuo wanavianika visima vyao juani na hata kukinya hawavianui, eti utamu wa maisha huo.

Tazama matokeo yake. Vijusi kupengwa kama kamasi tena mbele ya umma. Baada ya kujivinginya kwa raha kule chumbani mkiwa na yule bwana, baada ya kurambana midomo  kama ndege anayelisha makinda, baada ya kuona kheri kulala chini yake chali huku akitingiza kiuno chake kama mkia wa kondoo aliyenona akimbiapo kwenye mteremko;hatimaye ukapata kifundo ulichokichumia. Kisimani mkaangushwa mbegu za uhai. Kilicho na uhai hukua, kijusi kikajengeka panapostahiki ila unaamua kukipenga baada ya kugundua kuwa si cha mtu maalum.

Wakati mwingine ni heri mbwa koko kuliko mwanamke 'aliyelazimishiwa uhuru'. Mbona hivyo? Ni kuwa mbwa koko hata apandiwe na mbwa wa kiume zaidi ya elfu moja, atatunza mimba na kuzaa wana. Mbwa koko haavyi mimba, mbwa koko hana 'mtu' maalum. Mbwa koko, hauwi vijusi. Mbwa koko hudhamini maisha ya kiumbe alichobeba kwa hiari. Taamali hayo. Hewala

No comments:

Post a Comment