ONLINE

Friday 4 March 2016

KITUMBUA CHAINGIA MCHANGA BUNGOMA


By SIMIYU Wanyonyi

Tarehe 27 ya februari ilikuwa ni siku ambayo wanazuo kutoka Bungoma walijawa na furaha ghaya kutokana na ziara ya waziri wa elimu, utamaduni na spoti katika kaunti hiyo Bi Berril Mutekhele. Wanafunzi hasa waliohudhuria mandhari hayo walifurahi baada ya waziri kutuza juhudi zao kwa kopola maji kwa hisani ya koo zao.

Shamrashamra ziliendelea hadi kufikia siku ya jumatatu ambapo meli ilianza kuyumbayumba. Makubaliano yaliokuwepo siku ya jumamosi yalikuwa kwamba angalau kiasi cha shilingi elfu kumi zilizotolewa na Bi Mutekhele zingehifadhiwa kwenye hazina ya chama cha MUBSA ili ziwe akiba ambayo siku zote haiozi. Lakini je, hayo yalitekelezwa?

Duru za kuaminika ni kuwa ni shilingi elfu tatu na miatano pekee ndizo zilizo kwenye akiba ya chama kinyume na makubaliano. Ikumbukwe kuwa kati ya shilingi elfu sabini zilizotolewa na waziri, shilingi mia tano kila aliyehudhuria. Idadi kamili ya wale waliohudhuria kulingana na wadaku wangu ilikuwa kati ya watu 64 na 67 pekee. Ukizingatia idadi hiyo, shilingi zisizozidi elfu thelathini na nane ziligawiwa wanazuo hao huku pesa zote zilizosazwa zikibaki mikononi mwa Rais wa chama Bw. Werunga Wisdom.

Mshikeshike ulizuka jana katika mkutano wa kila wiki kwenye ukumbi wa NCT7 baada ya kusomwa kwa makadirio ya pesa hizo. Kulingana na makadirio ya Rais, yamkini wanazuo 106 bali si 64 hivyo mgao ulikuwa hamsini na sita elfu ingawa awali kwenye mtandao wa Whatsapp alikuwa amedai ni idadi ya wanazuo 112 ndio waliohudhuria. Vile vile, alidai kuwa kila kiongozi alipewa shilingi elfu moja kila mmoja jambo ambalo baadhi ya viongozi walipuuzilia mbali wakisema walipewa idadi sawa na wanachama.

Swala lilotia watu tumbo joto ni kupotea kwa zaidi ya shilingi elfu ishirini zinazodaiwa zilikuwa mikononi mwa mwenyekiti.

Alipokazwa kwenye koo ili kutoa mwanga wa jinsi pesa hizo zilipotea, mwenyekiti Bw. Werunga alitishia kujiondoa kwenye wadhifa huo huku akidai kuwa hana chakupoteza kwani yeye si mkaazi wa kaunti ya Bungoma bali ni wa Trans_nzoia. Kamati ya watu kumi ikiongozwa na Bw. Nickson Barasa ambaye ndiye aliyemwalika Bi.Mutekhele ilibuniwa kwa ghafla ili kufanyia uchunguzi wa kina kuhusu makadirio ya pesa hizo. Mwenyekiti wa Chama pamoja na uongozi wa MUBSA wamepewa hadi jumamosi wiki hii kukadiria kupotea kwa pesa hizo la sivyo wachukuliwe hatua ya kisheria kando na kuwashurutisha wajiuzulu.

Inaaminika kuwa viongozi wa MUSO;Elsie Muhonja ambaye ni naibu mwenye kiti na Oliver Bill ambaye ni mwanasheria wa MUSO wamefahamishwa kuhusu uwezekano wa kuombwa usaidizi wa kisheria na wakaahidi kusaidia ilikikukinusuru kitumbua.

No comments:

Post a Comment