By YASSINA Terry
Umeneja ni wa nani Stamford Bridge?
Huenda Chelsea ikamteua Antonio Conte kama meneja mapema mwezi ujao, huku meneja huyo wa Italia akiwasili baada ya mechi za Euro 2016.
Conte ana imani kuwa atawapiku wapinzani wake; Diego Someone na Massimiliano Allegri katika kuchukua usukani kule Stamford Bridge.
Hata hivyo, meneja wa Manchester City, Manuel Pellegrini ameibukia kuwa mpinzani mkuu wa Conte wakati Chelsea ikiendelea na pilka pilka za kumnasa meneja mpya.
Conte amekwisha taja kiungo wa Roma, Radja Nainggolan na Paul Pogba kama baadhi ya nyota atakaowasajili akichukua hatamu kule Stamford Bridge. Ripoti zipo kuwa Conte ambaye aliwahi ichezea timu ya taifa ya Italia kama kiungo wa kati, huenda akasafiri na mkurugenzi wa Roma, Walter Sabatini iwapo ataelekea Chelsea.
Chelsea inaendelea kutafuta kocha kando na Conte huku meneja wa Chile Jurge Sampaoli na meneja wa Juventus Massimiliano Allegro wakifuatiliziwa zaidi.
Tetesi Nyinginezo
Real Madrid inazingatia suala la kumwuza Gareth Bale mwezi Juni kufuatia rekodi mbaya ya majeraha ya mchezaji huyo ambaye ameshiriki mechi chache mno.
Huenda kiungo na aliyekuwa nahodha wa Arsenal, Mikel Arteta akatunukiwa kazi ya umeneja kule Manchester City na Pep Guardiola iwapo Mhispania huyo ataamua kustaafu mwishoni mwa msimu huu.
Mshambulizi wa Manchester city, Sergio Aguero ametia sahihi kandarasi mpya na klabu hiyo .Kandarasi yake ya sasa imeongezewa kwa mwaka mmoja
Meneja wa Ujerumani, Olivier Biehoff amemkashifu Louis van Gaal kwa kutomjali Bastian Schweinsteiger ambaye amo mkekani kwa jeraha la uvungo wa goti .Van Gaal atashikilia hatamu kama kocha wa United hadi mwishoni mwa msimu huu kwa kuwa Jose Mourinho amekataa kuchukua hatamu katikati ya msimu.
Sunderland inatilia manani kumsajili mlinzi wa Lille, Adama Soumaro wakati meneja Sam Allardyce akijaribu kuimarisha matokeo ya timu hiyo.Black Cats wamo kati ya timu tatu za chini kwenye jedwali la ligi kuu.
Mshambulizi wa Borussia Dortmund, Pierre Emerick Aubemeyang amekiri kuwa alikataa kujiunga na Newcastle United misimu miwili iliyopita.
No comments:
Post a Comment