ONLINE

Tuesday 27 June 2017

SIMBA MAGHUFULI

Hoja ya Rais wa jamhuri ya Tanzania Dr. Maghufuli kuwa Wasichana wanaoshika mimba wakiwa shuleni wakatiziwe masomo hapo kwa hapo imeteka anga za Afrika mashiriki huku wenyeji wakiwa na mitazamo na maoni anuwai kuhusiana na swala hili. Wengi wao, wakiwemo watetezi wa haki za binadamu na wanawake wasomi wametaja mawazo hayo ya Rais Maghufuli kama yasiyofaa na yanayolenga kumpokonya mtoto wa kike haki ya kupata elimu


Kwa maoni yangu binafsi, nadhani hoja hii inafaa kushabikiwa na kutekelezwa siyo katika mtalaa wa elimu wa Tanzania tu, bali hata Afrika mashiriki kote ukizingatia kizazi maluuni cha sasa; Kizazi ambacho mzazi amekosa kumwajibikia mwanawe. Mzazi wa kizazi hiki amemwachia mwalimu (mzazi wa shuleni)  kazi ya malezi.

Fikiria hivi; mtoto wa umri chini ya miaka minane anahudhuria 'disko matanga' badala ya kuwa nyumbani akisoma au akilala. Hili linadhihirisha tu jinsi ambavyo wazazi wametepetea kuwapa wanao ulinzi. Pia, wazazi wanakosa kuwajibikia jinsi wanao wanavyovaa. Swala kuu katika mavazi siku hizi za leo huwa ni kuambatana bega kwa bega na mitindo ya dunia na hasa sana kuiga uzungu. Jambo hili huwaweka watoto hawa wa kike katika hatari ya kubakwa ikiwa si kuamsha ashiki za wanaume wanaonza kuwaandama kama nzi na kidonda kilichowachwa wazi na Sote tunajua, ukigota gogo utasikia mlio.

Hoja hii ya Rais Maghufuli itamkumbusha mtoto wa kike  kujua kuwa ana wajibu wa kujilinda ikiwa anataka kutengeza mustakabali wake kielimu na maisha kwa upana. Isitoshe, Kwa upande wa Wazazi, hoja hii itawakumbusha majukumu yao kwa mtoto msichana hasa akiwa likizoni.


Hapa kenya yamkini msichana maadamu ni mwanafunzi ati, hata akiwa mja mzito anapaswa kuendelea na masomo bila kukatizwa. Jambo hili linatendeka sana katika shule za kutwa zinazopatikana mashinani. Fikiria mfano ambao mwanafunzi mwenye mimba anatoa kwa vichekechea na wasichana wengine waliochini yake kiumri. Visa vya ufuska miongoni mwa watoto wasichana vitaendelea kwa dhana kuwa hata ikiwa atafanya ngono, atalea mimba, azae na arejee shule. Kizazi kitazuka ambapo hata makanisa yanayotafuta watawa yataathirika  kwa kuwa kupata bikira kutakuwa sawa na kumtafuta samaki hai katika Nchi kavu. Fikiria jina la shule anayosomea na walimu wake. Wanafanya shuleni, ambapo panafaa pawe mahali pa kurekebisha na kunyoosha tabia za mwanafunzi pawe kama mahali panaposhabikia na kukuza ufuska. Walimu watadunishwa na kuitwa wakiritimba kwa kuwapa maadili wana wao nyumbani eti na kuwapuuza wasio wao, ambao wanawafundisha shuleni.


Sifai kutaja kuwa suala hili litapunguza viwango vya uaviaji mimba miongoni mwa wasichana wa shule, lakini pia, ikiwa ufuska utapunguzwa kutokana na mtoto msichana kuwajibikia mwili wake pamoja na wazazi kurejelea malezi yao ambayo zamani yalijaa lulu za maadili pamoja na sheria kali za kuwalinda dhidi ya fisi hili kwa jina la ngono linalowaotea pindi wanapobalehe, haiwezekani tatizo hili litapunguzwa pia.

Tukilikashifu suala hili, pia inafaa tukumbuke kuwa Chui, pamoja na ukalu wote, huwa na mke na wana.


@kaka siwa