By YASSINA Terry
Wako wapi mibabe waliovuma enzi hizo?
Msimu wa elfu mbili na tatu hadi ule wa elfu mbili na nne utasalia kwenye vitabu vya historia. Ni katika huo mwaka ambapo Arsenali ilinyakua kombe la ligi kuu ya Uingereza bila kupoteza mechi yoyote. Swali ni je, mibabe waliotwaa ubingwa huo walielekea wapi? Bado wanashughulika na masuala ya kabumbu au la?
Ushindi wa kikosi hicho hautawahi sahaulika. Baadhi ya nyota waliovuma katika msimu huo ni Thierry Henry, Patrick Vieira, Dennis Bergkamp miongoni mwa wengine wengi. Wanne kati ya mibabe hao wangali wanacheza, watatu wamejitosa katika umeneja ilhali wengine wanejimwaya katika vyonbo vya habari, biashara na hata siasa.
Jens Lehmann: baada ya kugura Arsenali mwaka wa elfu mbili na nane kuelekea Stuttgart alirejea London mwaka wa elfu mbili na kumi na moja japo kwa muda mfupi. Mechi ya Arsenali dhidi ya Blackpool, ambayo Arsenali walishinda mabao matatu kwa moja ndiyo iliyokuwa ya mwisho katika taaluma yake. Hivi sasa yuko katika kituo cha televisheni kule Ujerumani.
Ashley Cole: aliondoka Arsenali na kuelekea Chelsea ambako alishinda mataji manne ya FA, ligi ya mabingwa na ile ya Uropa. Baada ya kuondoka Stamford Bridge, Cole alienda Roma na baadaye kujiunga na LA Galaxy ambako anacheza hadi sasa.
Sol Campbell: aligura Arsenali kuelekea Portsmouth, kisha akajiunga na Notts County kabla ya kurejea Arsenali mwaka wa elfu mbili na kumi. Campbell alielekea Newcastle United msimu uliofuata na ambao ulikuwa wa mwisho kwa taaluma yake. Hivi sasa amejitosa katika siasa.
Kolo Toure: aligura Arsenali na kuelekea Manchester City mwaka wa elfu mbili na tisa. Toure, kisha alijiunga na Liverpool mwanzoni mwa msimu wa elfu mbili kumi na tatu hadi kumi na nne.
Lauren: aliichezea Arsenali kwa miaka sita na baadaye akajiunga na Portsmouth kama Campbell. Alikamilishia taaluma yake kule Uhispania; Cordoba na hivi sasa anafanya kazi katika televisheni ya Sky Sports.
Robert Pires: aliichezea Arsenali misimu sita na kuelekea Villarreal mwaka wa elfu mbili na sita. Pires alirejea Uingereza katika Aston Villa na baadaye akajiunga na Fc Goa ya India. Alitangaza kustaafu kwake wiki iliyopita.
Patrick Vieira:alikuwa nahodha wa mibabe hao na aliondoka Arsenali kuelekea Juventus alikoshinda taji la Serie A. Baadaye alijiunga na Inter Milan kabla ya kukamilishia taaluma yake Manchester City. Hivi sasa ni mmoja wa mameneja wa klabu ya New York City.
Thierry Henry: ni mfungaji bora zaidi katika historia ya Arsenali. Alijiuga na Barcelona kabla ya kurejea Arsenali mwaka wa elfu mbili kumi na mbili. Hivi sasa anafanya kazi na kituo cha televisheni ya kabumbu Sky Sports.
No comments:
Post a Comment