By Yassina Terry
Nyota katika mbio za magari ya langa langa Louis Hamilton amesema kuwa Ferrari itang'aa katika mashindano yatakayoandaliwa kule Australia. Ingawa dereva wa Ferrari, Sebastian Vettel amesisitiza kuwa Mercedes ndio mabingwa wa sasa kabla ya shindano la Grand Prix, Hamilton ameonya kuwa Ferrari almaarufu "Scuderia" watadhibitisha ubabe wao.
Kampuni ya Ferrari, hata hivyo, haijatoa taarifa yoyote kuhusiana na uwezo wao wa kung'aa katika Grand Prix kule Melbourne, lakini bingwa wa Formula 1, Louis Hamilton anahisi kwamba kampuni hiyo inajidunisha kwa hiari. Aidha, nyota huyo ameongeza kuwa wamekuwa na rekodi mbovu hivi karibuni lakini ana imani wataibuka mabingwa.
Nico Rosberg wa Mercedes, amesema kuwa Ferrari ni tishio kubwa ikizingatiwa kuwa katika shindano la hivi majuzi, Mercedes walishinda kwa tundu la sindano, huku Ferrari wakiwakaribia kwa sana. Rosberg amekiri kuwa sharti wawe makini wakati huu.
Mpinzani wa Hamilton, Sebastian Vettel amesema kuwa Mercedes ndio nyota katika mbio hizo lakini Ferrari imo katika juhudi za kutwaa ubingwa huo.
Mikwaruzano ya mabingwa
Itakuwa wikendi machachari kabisa kwa mashabiki wa ligi maarufu zaidi duniani, yaani ligi ya Uingereza, huku wengi wakitarajiwa kutia ndoana katika Sport Pesa, Betway na kadhalika. Baadhi ya mechi zitakazosakatwa ni;
Jumamosi
Everton vs Arsenal
C. Palace vs Leicester
Watford vs Stoke
W.Brom vs Norwich
Chelsea vs West Ham
Swansea vs A. Villa
Jumapili
Southampton vs Liverpool
Newcastle vs Sunderland
Man city vs Man united
Tottenham vs Bournemouth
No comments:
Post a Comment