ONLINE

Friday 18 March 2016

UKUMBUSHO WA WAATHIRIWA WA GARISSA KUFANYIKA


By Wanyonyi Simiyu

Makumbusho ya wanazuo walioangamia kwenye vamizi la kutisha lililofanyika kwenye Chuo kishirikishi cha Moi bewa la Garissa umepangwa kufanyika mwezi kesho. Kamati iliyoteuliwa kupanga mikakati ya ukumbusho huo ilikutana jumannekwenye ofisi ya mdiri wa wanafunzi ili kuhakikisha ufanifu wa ukumbusho huo. Tarehe mbili Aprili ndiyo tarehe iliyopangwa.

Katika mkutanohuo, shughuli mbalimbali zilipendekezwa kufanyika siku hiyo.Baadhi ya shughuli hizo ni kufanyika kwa mkutano wa maombi utakaoongozwa na shirika la FOCUS KENYA. Upanzi wa miti kama kitambulisho cha walioaga pia umepangiwa kufanyika.Vile vile kuna viongozi wa kitaifa ambao wataalikwa kwenye ukumbusho huo.

Kamati ya wanafunzi ilijumuisha wawakilishi wa uongozi wa MUSO na waliokuwa viongozi wa chuo hicho kabla kutokea kwa kisa hicho. MUSO iliwakilishwa na Elvis Langas huku uongozi wa Garissa ukiwakilishwa na Steve Mwangi ambaye alikuwa katibu mkuu, Collins waliaula Wetangula ambaye alikuwa naibu mwenyekiti, Daniel Kinuthia ambaye alikuwa mkurugenzi wa fedha na Jomo Samuel ambaye alikuwa msimamizi wa michezo. Mashirika ya FOCUS KENYA na DIPAD pia yaliwakilishwa.

Kando na hayo kutakuwa na kuzinduliwa kwa vitabu kutoka kwa Daniel Kinuthia na Clinton Odhiambo ambavyo vimefungamanishwa na matukio yale ya Garissa. Vile vile msanii Brian maarufu kama Bradfyter anatarajia kuzindua wimbo mpya wenye maudhui ya yaliotokea.

Wanamgambo wa Alshabab walivamia chuo kikuu cha Moi bewa la Garissa na kuwaua watu 147 ambao wengi walikuwa wanafunzi. Zaidi ya wanafunzi 500 walinusurika huku 79 wakipata majeraha.

No comments:

Post a Comment