ONLINE

Saturday 19 March 2016

PENGO LAJAZWA MUSO

HELLEN BRAHANE: kiongozi shupavu wa MUSO aliyegura masomo Moi Kuenda Australia.
Na JOMO Samuel

       Ni bayana kuwa mmoja wa viongozi wa MUSO waliochaguliwa mwaka jana aligura Chuo Kikuu cha Moi.Mkurugenzi huyo aliyehudumu katika kitengo cha maakuli aliangukiwa na nyota ya jahaa mbapo inakisiwa kuwa alipata ufadhili kwenda kuendeleza masomo yake katika nchi ya Australia.kupitia kwa mitandao yaWatsapp na Facebook aliwaaga wanazuo na kuwapa shukrani kwa kumchagua kama kiongozi na hatimaye kuwatakia kila la heri.

      Kwa mujibu wa katiba ya MUSO kipengee kinachohusu uchaguzi;Kiongozi yeyote anapotoka ofisini nafasi yake inastahili kutangazwa wazi na uchaguzi mdogo kufanywa.Duru za kuaminika ni kuwa nafasi hiyo haikutangazwa wazi.Florida aliyekuwa wa pili katika kinyang'anyiro hicho uchaguzi wa mwaka uliopita aliteuliwa kujaza pengo hilo.Inakisiwa kuwa ikiwa uchaguzi mdogo ungefanywa ungekadiria upungufu wa pesa ambazo zingetumiwa kwa miradi mingine iliyo na manufaa zaidi.Kutokana na ratiba ya muhula, masomo pia yangeathiriwa maanake muhula u katikati;muda mwingi wa masomo ungepotezwa kwa kampeni.Jambo ambalo lingesababisha muhula kuongezwa.

      Licha ya kufanya uteuzi huu, ni wachache wanaofahamu jambo hili.Hii ni ishara bainifu kuwa kuna ukosefu wa mawasiliano kabambe kwa wanaostahili kuliwajibikia jambo hili.Wengi wamesalia kusema kuwa nafasi hiyo i wazi;kutokana na juhudi zetu za cfhapisho la "The Legacy" nimewapa hali halisi ya mambo kuhusu muungano wetu wa MUSO.

      Katika mawasiliano kwa njia ya simu na mkurugenzi mpya Florida Mukiri, alisema kuwa ana furaha kwa uteuzi aliopata.Alidhibitisha kuwa kazi hiyo ameichukuwa kwa moyo mkunjufu na atafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa matakwa ya tumbo ya wanazuo yametiliwa maanani.

     Kila la heri Florida ila kumbuka ahadi ni deni. Jomo Samuel

No comments:

Post a Comment