ONLINE

Saturday 19 March 2016

AL-SHABAAB TOKENI!!



Na: George Mwangi Maina.

Machozi yatiririka, kupukupu yanirowa

Huzuni kikombe tele, kenda zake mpenzi

Tangulia mwaka Jana, chuo kikuu Garissani

Bunduki kaonyeshewa, ikawa ndo mwisho wake

Alshabaab tukomeni!


N'likupenda kwa dhati,ya mtima wangu wote

Hakika sijadiriki, ndoo umepiga teke

Kwa nini uliniacha, ghafla we kipenzi

Simanzi na upweke,salio langu daima

Alshabaab tukomeni!


Hakika 'asali' yangu, huba zetu 'tazilinda

Sinayo nia nyengine, ya kutafuta mwengine

Japo umetangulia, niko nawe buriani

Dawa yangu ya penzi, kwaheri ya kuonana

Alshabaab tukomeni!


Huba zisizo kipimo, daima 'tazikumbuka

Kipenzi tulipatana, Garissa tukapendana

Tukafunga urafiki, Wa kudumu aushini

Tukaasi upwekee, nazo huba zikazidi

Alshabaab tukomeni!


Alshabaab wakaja, mtutu kakumaliza

Ulipojijajiisha, kutoasi dini yako

Bunduki kaonyeshewa, 'kafyatuliwa risasi

Kipenzi wasamehe, Jalali 'takuzawadi

Alshabaab tukomeni!


Wamwaga damu nyie, machozi mwaniletea

Mbona mkammaliza, tegemeo la aila

Mwaniletea ukiwa, na upweke wa daima

Kwaheri ya kuonana, mpenzi mwenye huba

 Alshabaab tukomeni!


Mamako akulilia, Alshabaab 'la'ni

Aprili tarehe mbili, 'tabakia kumbukizi

Uchungu ulipitia, wa mtutu kichwanii

Mpenzi ulikufa, sababu hamnaazo

Alshabaab tukomeni!


Hakika nimeghairi, sitopata mwengineo

Shanga mingi ulonipa, hifadhi la pendo letu

Taziliinda daima, ukumbusho wako kwangu

Dunia rangi rangire, hakika rangi rangire

Alshabaab tukomeni!


Naani kawadanganya, bikra sabini tapata

Mfikapo mbele zake, Jalali tawahukumu

Nyie wauaji insi, pamoja mtachomeka

Kwenu daima dawama, nyie wamwagaji damu


Alshabaab tukomeni!

5 comments:

  1. Hill tendo la uwoga lisiwahi tendeka tena tunapoishi. Buriani wenzetu.

    ReplyDelete
  2. Hill tendo la uwoga lisiwahi tendeka tena tunapoishi. Buriani wenzetu.

    ReplyDelete
  3. Too early to mension such a sad moments. Hold it

    ReplyDelete
  4. @James,they'll always remain in our hearts
    Fare thee well

    ReplyDelete